Mahakama kuu kanda ya Mwanza imetupilia mbali mapingamizi ya kisheria yaliyowekwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na mwanasheria mkuu wa serikali, kwamba mtoa maombi katika kesi hiyo ya madai namba 10 ya mwaka 2015 Bw.Charles Lugiko ambaye ni baba mdogo wa marehemu Alphonce Mawazo hana uhalali wa kisheria wa kuwasilisha maombi hayo kwa vile yeye si baba mzazi wa marehemu.
CHANZO: ITV

 
Top