Chama cha wamiliki wa daladala jijini Dar es Salaam-Darcoboa- kwa
kimepanga kuhacha kuwatoza walimu wote wa shule za msingi na sekondari
za serikali katika manispaa ya Kinondoni kuanzia machi 7 mwaka huu ikiwa
ni kuungamkono uamuzi wa rais Dkt John Magufuli wa kutoa elimu bure kwa
wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa
Darcoboa Bwana Said Mabrouk amesema walimu wa shule za msingi na
sekondari za serikali hawatotoza nauli kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa 2
asubuhi na wakati wa mchana ni kuanzia saa 9 hadi saa 11 jioni, na
kusisitiza ambapo ametaka hamalshauri za manispaa kuweka utaratibu
maalum wa vitambulisho vitakavyokuwa na picha za walimu hao.
Aidha akizungumza katika mkutano huo, mwenyekiti wa umoja wa
wasafirishaji mkoa wa Dar es Salaam Bwana William Masanja amevitaka
vyombo vya habari kutoa ushirikiano wa kutangaza mpango huo wa wamiliki
wa daladala, umoja wa wasafirishaji, chama cha wafanyakazi
madereva-Tadwu na serikali ili kuwawezesha walimu kufahamu wa shule za
serikali kutambua fursa hiyo.
Chanzo: ITV