RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 28, 2017 amepokea rasmi taarifa ya Uhakiki wa Watumishi wa Umma nchini wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Akikabidhi taarifa hiyo kwa Rais Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Rais amesema kuwa, Wizara yake iliagiza NECTA kuhakiki vyeti vya kidato cha nne, cha sita na vya uwalimu.


“Jumla ya watumishi wa umma 435,000 wamefanyiwa uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma, Watumishi 9932 kati ya watumishi waliohakikiwa walikutwa na vyeti vya kughushi, Vyeti vyenye utata. Vyeti 1538 vilikuwa vikitumiwa na jumla ya watu 3076”


Akihutubia baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli amewataka watumishi 9,932 waliobanika kuwa na vyeti vya kugushi waondoke kazini mara moja, na kuagiza mamlaka zilizowaajiri kukata mishahara yao huku akiongeza kuwa kwa wale watakaobakia kazini hadi Mei 15, wakamatwe ili sheria ichukue mkondo wake ikiwemo kufungwa jela miaka 7.

“Mtu aliyeghushi vyeti hatuwezi kumsamehe, wote ataondoka mara moja, mishahara yao ikatwe kabisa”

“Hao watumishi 9,932 wenye vyeti feki wenyewe kazini mara moja, watumishi wenye vyeti feki ambao watakaidi na kubaki kwenye ajira hadi Mei 15, wakamatwe wafikishwe kwenye vyombo vya sheria wafungwe hiyo miaka 7.

 “Wanaotumia cheti kimoja watu wawili, wasiwekewe mshahara ya mwezi huu, na kama wanajijua wajisalimishe, pia nikuombe Waziri utangaze mara moja nafasi za kazi 9,932 za watumishi wenye vyeti feki ambao wametakiwa kuondoka mara moja kazini ili zichukuliwe na watu wengine wenye vigezo.” Alisema Rais Magufuli

http://studentswagas.blogspot.com

 
Top