Vijana wanaotambulika kwa jina la Panya road maeneo ya
Kigogo wameanzisha kitimtim Jana jumatano baada ya kijana mwenzao, Rama (dogo
Rama) kuuawa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za wizi maeneo ya
Sambusa.
Vijana hao wenye umri kati ya 12, 13, na 14, wameanzisha
vurugu hizo jana wakati watu walipokuwa wanaelekea kwenye mazishi ya kijana
mwenzao aliyeuawa. Kwa mujibu wa wananchi waliokuwa wanatoa maelezo yao kwenye
kipindi cha Hekaheka redio Clouse FM, wanaeleza kuwa vijana hao walikuwa
wanawaibia watu njiani wakiwemo waliokuwa wanakwenda kwenye mazishi na hata
waliokuwa wanapita njia.
Baada ya mazishi vijana hao walifunga mtaa wa Sambusa kwa
kufanya vurugu ikiwemo kuharibu mali za watu pamoja na kuwapiga watu wote
waliokuwa wanaonekana mtaani hapo. Vurugu hizo ziliendelea hadi walipofika
askari polisi na kuwatuliwa vijana hao.
Kwa taarifa na tetesi zinazosambaa wakati huu ni kwamba
vijana hao (Panya road) wapo Tabata wanajipanga kwaajili ya kurudi tena mtaani
kuendeleza mashambulizi.