Wanasayansi wanasema kutoa ushuzi ni afya
Kila mmoja wetu kwa wakati fulani huhisi kuvimbiwa na gesi
nyingi tumboni.
Suluhu ya pekee hapa huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni
Sasa Wanayansi katika chuo kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa
wamegundua harufu mbaya kama vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua, ina
manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.
Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya
magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani.
Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako
inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.
Ndio! athari ni kile ambacho unakidhania: Eti watu wanauchukulia utafiti huu
kumaanisha kuwa harufu mbaya inayotokana na mtu kujamba inaweza kuzuia magonjwa
fulani mwilini kama vile Saratani.
Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua
kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana katika
Mayai yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.
"ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na harufu mbaya na
hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na harufu ya mtu kujamba, hutengezwa
mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa magonjwa fulani, ''asema Daktari Mark
Wood,Profesa wa chuo hicho cha Exeter.
Gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa
utafiti huo.
Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya kujamba kuchukiza, ina uwezo
mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu kupatwa na magonjwa kama vile,
Saratani,Kiharusi, mshtuko wa Moyo na kuumwa na mifupa