Katika hali ya kushangaza ambayo imekuwa ikijitokeza katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania hasa maeneo ya Dar es salaam, Kibaha, na Kahama. ambapo kondomu za kike zimekuwa zikitumika kama mapambo kwa wanaume na wanawake

Wote wanaume kwa wanawake wamekuwa wakivaa bangili zilizokuwepo kwenye kondomu za kike kama mapambo. Bangili hizo ambazo zinanyofolewa kwenye kondomu za kike zimekuwa zikiuzwa kwa gharama ya shilingi 2000/=

Kondomu hizo ambazo zimetengenezwa kwa madhumuni ya kumlinda mwanamke wakati wa kufanya tendo la kujamiiana, zimeonekana kutumika kinyume kabisa na malengo.

Hali hiyo inaashiria kuwa ipo kazi nzito sana ya kupambana na maambukizi ya virusi vinavyoeneza Ukimwi (VVU).

 
Top