https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_pDD0Gr8s1qMdD2AEx_MnF_mw7mTeZEDG7wiYTJ4Bk-jwgdGttdvMj5PGnqoBb-Y7GXwTASIDLzXR8Adh6pC6ZTqfVdyUOkf4PZoN2TWss_kqry_8SnrDeqVegernNek00xItHCP4iJOc/s1600/unnamed2.jpg
       Askari wa jeshi la polisi wakiangalia mabaki ya watu wawili waliochomwa moto kwa tuhuma za wizi

Asubuhi ya Jumamosi, vijana wawili wamejikuta wakipoteza maisha baada ya kuchomwa moto kwa tuhuma za wizi wa pochi huko Tabata Liwiti jijini Dar es salaam.



Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa vijana hao walikuwa wakifanya jaribio la kuiba pochi kwa mwanamke mmoja kwa kutumia usafiri wa pikipiki, ambapo wananchi waliwafukuza kutokea pande tofauti na kuwatia nguvuni.

Wananchi wenye hasira kali waliwapiga watu hao na mwisho kabisa walichukua jukumu la kuwatia moto huku wakidai kuwa hiyo ni dawa pekee kwasababu mara nyingi watu wa namna hiyo wanapofikishwa katika vyombo vya dola, huachiwa huru baada ya siku kadhaa.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2OxLpIe9XFr2Xvu18JXc77B-JJeY8Bldn6KdHADb8qGkIOFt1wWx5tOjyp60nFtNc_XhDEP8oNXNM9mmtzn3qpKUWcGVGCDfrodbPwy6Arh-qdSOY0UGpJG0OMXKTt1wZsoWtoMf8ga_K/s1600/unnamed1.jpg Askari wakipakiza kwenye gari miili ya watu wawili waliochomwa moto


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh1h0GTInWtrC7OHI6jZLLkbET5yh6T8MPM00pRZ8uh8haZXFl8hNdb3CqyZ-NZtCSpyN5GK2nVtXahfo33uXajTCBnvy64TIOzHHVVJ9TRlpUe9xg5wwgEugi5lnbMjtZ8cMG2byCr7QjU/s1600/unnamed3.jpg                                                     
Pikipiki inayodaiwa kutumiwa na watu hao katika zoezi la wizi
 
Top