Mtoto wa mwezi mmoja ameshambuliwa na panya wakati mama yake
alipokuwa nje akifua na kumuacha mtoto wake ndani amelala.
Mtoto Erena ambaye amepatwa na masahibu hoyo ya kung’atwa na
panya maeneo ya puani na pamoja na vidole vyake vitatu vya mikono huko
Alexandra, Johannesburg anasubiri kufanyiwa upasuaji kwaajili ya kurekebishwa
maeneo ya uso wake yaliyoathirika.
Mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa nje akifua wakati mtoto
wake akishambuliwa na panya hao, alisema kuwa aliingia ndani ghafla aliposikia
harufu ya damu, na lipofika ndani alimkuta mtoto wake huyo tayari amekwisha
jeruhiwa.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kimeeleza kuwa tukio
hilo la panya hao waliokuwa na ukubwa usio wa kawaida wamekuwa na kawaida ya
kuwauma watoto na wazee katika eneo hilo kulingana na kutokuweka safi mazingira
yao