Mheshimiwa jakaya mrisho kikwete amezungumza na wanafunzi wa
Mzumbe na kueleza kuwa serikali ipo katika mpango wa kufuta ada katika elimu ya
Sekondari.
Mheshimiwa amesema kuwa serikali imeadhimia kufanya hivyo
ili kuwawezesha watanzania wengi wamalize elimu ya sekondari bila vikwazo vya kiuchumi.
Hivyo watanzania watakuwa na nafasi ya kupata elimu pasipo
kutoa malipo yoyote kuanzia elimu ya msingi hadi ngazi ya Sekondari.
Ameongeza kwa kusema kuwa shule za kata zimeweza kuleta
mafanikio makubwa sana katika jamii ya watanzania. Kwa namna hiyo ni serikali haina budi kuboresha zaidi sekta ya elimu kwa kuondoa karo za sekondari.