Wakati mgumu waliokuwa nao Yanga wa kutaka kumtema Okwi umetoweka ghafla na kupatikana hali ya uhuru na urahisi kwa timu hiyo.


Hali hii imetokea pale Yanga ilipokuwa ikitamani kumtema Okwi na kubaki na Kiiza kutokana uongozi wa timu hiyo kuto kufurahishwa na usumbufu wa Okwi. Hata hivyo timu hiyo ililazimika kufanya mpango wa kumtema Kiiza kufuatia masharti ya kuvunja mkataba wa Okwi kuwa magumu zaidi kuliko masharti ya kuvunja mkataba na Kiiza.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii huko Uganda kimeeleza kuwa, Okwi sasa hivi amekuwa akigombaniwa na klabu mbili za Ulaya ambazo zinapatikana katika nchi za Australia na Sweden.

“Okwi hawezi kuja huko sasa, kuna mambo tunashughulikia, kuna klabu mbili za Ulaya zinataka kumsajili wapo tayari kuwapa fedha nyingi Yanga kama wakikubali kumtoa, nafikiri hilo ndiyo litakuwa jambo jema kwa Yanga ambao wanaonekana kutokuwa na furaha naye,” Kilieleza chanzo cha habari.

Hivyo kitendo hicho kimeonekana kuleta mteremko kwa Timu ya Yanga kuweza kubakia na Kiiza pasipo kukumbana na vikwazo walivyokuwa wanaviogopa.

 
Top