Polisi waliwasiliana na wakazi wa eneo hilo ili kuona kama
kuna taarifa zozote za kupotea ama kumezwa kwa mtu yoyote na nyoka huyo.
Nyoka mkubwa amepatikana kwenye ziwa Proctor, kusini mwa
Carolina. Kwa mujibu wa mtu mmoja anaye kula nyoka amesema kuwa nyoka huyo
alikuwa na urefu wa futi 98.
“Sidhani kama nyoka huyo ni mkubwa kama ambavyo inaonekana
kwenye picha, Mimi nadhani picha hiyo imekuzwa kutokana na engo ya mpigapicha
aliyeipiga” alisema mtu mmoja ambaye alishuhudia picha hii baada ya kuiona
mtandaoni.
Hata hivyo nyoka huyu bado ni mkubwa sana, na rangi ya ngozi
yake inaonesha kuwa anafanana kabisa na nyoka wanaopatikana Kusini Mashariki
mwa Asia.
Baada ya kuperuzi kwenye mtandao wa Google, jibu la asili ya
nyoka huyo limepatikana kuwa ni nchini Indonesia, na baada ya kuperuzi zaidi
ikabainika kuwa nyoka huyu alipatikana karibu na kijiji cha mji wa Belinyu.
Kupatikana kwa nyoka huyo kulitokana na watengeneza barabara
kupasua gogo lililokuwepo pembezoni mwa barabara. Nyoka huyo alikuwa
amejihifadhi ndani ya gogo hilo. Hivyo walimtoa nyoka huyo akiwa tayari
amekwisha kufa na kuchukua jukumu la kumzika.