
Wakulima wa zao la Pamba wa Simiyu katika wilaya ya Bunda
mkoani Mara, wamejikuta wakipigwa changa la macho baada ya kupeleka mazao yao ya pamba
sokoni kwa lengo la kuuza.
Mtu mmoja ambaye aliyetambulika kuwa ni karani, alishiriki
kuwaingiza mjini wananchi hao (wakulima) kwa kununua pamba zao na kuwalipa kwa pesa
za bandia.
Baada ya wakulima hao kubaini utapeli wa mtu huyo, taarifa
zilifikishwa kwenye vyombo vya sheria ambako walimfuatilia mtuhumiwa na kumtia
mbaroni. Pesa hizo zilipokusanywa na wakulima hao zilipatikana noti ambazo
kama zingekuwa halali zingekuwa na thamani ya shilingi 200,00/=
Mtuhumiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi
zaidi ili kama akipatikana na hatia kuweza kuleta fundisho kwa watu wengine ambao wanajihusisha na
biashara haramu kama hiyo.