Kufuatia utafiti ambao umefanywa na chama cha wanawake
wanasheria (WLAC) mnamo mwaka 2012/2013 katika mikoa ya Kusini, imegundulika
kuwa asilimia 80 ya ndoa 100 zina matatizo na zinakabiliana na migogoro ya mara
kwa mara.
Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi wa WLAC Jane Magigita anasema
kuwa utafiti huwo ambao umefanyika mikoa ya Kusini kwa lengo la kubaini chanzo
cha kuvunjika kwa ndoa nyingi hasa katika maeneo hayo.
Anasema kuwa katika mashauri 20 ya ndoa ambayo huwasilishwa
kila siku kwenye ofisi za ustawi wa jamii, ni ndoa 5 tu ambazo hufanikiwa
kusuluhishwa na kurejeshwa katika hali ya kawaida.
Kwa mujibu wa Magigita ameeleza kuwa sababu kadhaa ambazo
zimekuwa zikipelekea ndoa nyingi kuvunjika ni pamoja na vitendo vya kikatili
ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia. Kwa mfano kupigwa mbele ya watoto, kuvuliwa
nguo hadharani na matusi ya kudhalilisha.
Stela Stephene ambaye ni Afisa ustawi wa jamii katika wila
ya Lindi, amesema kuwa kesi nyingi huishia kusuluhishwa katika ngazi ya
familia, na chache ndizo hupelekwa katika ngazi za juu.
Itaendelea kesho.....