Kocha huyo ambaye alishawahi kuifundisha timu ya Taifa
Stars, amesema kuwa kwa kutumia mbinu hiyo timu yake anayoifundisha itakuwa
bora na bora zaidi katika msimu wa ligi guu.
Alisema kuwa katika mazoezi ya kukinoa kikosi hicho kwaajili
ya maandalizi ya ligi kuu, atahakikisha kila mchezaji katika kikosi cha timu
hiyo anakuwa na uwezo wa kuchezea nafasi tatu tofauti pasipo kutetereka.
Kitendo hicho kitasaidi hata ikitokea mchezaji mmoja akawa
anaumwa ama ameshindwa kufika kwenye mechi kwa sababu zisizozuilika, haitakuwa
kikwazo mtu mwingine kuziba pengo lake.
“Ninataka soka la Kibrazili Yanga, kwa kuanza ninataka kila mchezaji awe na
uwezo wa kucheza nafasi tatu hadi nne.
“Hiyo itanisaidia mimi kama siku moja ikitokea mmoja majeruhi au ana kadi
nyekundu basi mwingine anachukua nafasi yake, pia itanisaidia kuleta changamoto
ya namba kwenye timu,” alisema Maximo