Shilikisho la soka la Tanzania (TFF) kupitia kamati ya tiba, limeeleza kuwa
katika msimu huu wa ligi kuu suala la kupimwa afya limetiliwa mkazo zaidi.
Hakuna mchezaji ambaye ataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo kama taarifa
zake za kiafya hazikupatikana.
Katika taarifa hizo shilikisho hilo limesema kuwa safari hii jambo hili
litatiliwa mkazo tofauti na misimu mingine iliyopita. Kwa lengo la kuhakikisha
usalama wa wachezaji wawapo uwanjani, kila mmoja atalazimika kupimwa afya yake.
Jambo hili limetiliwa mkazo hasa kwa wachezaji ambao ni wageni kutoka nje ya
nchi. Mara nyingi suala hili la kupimwa afya halikuwa likitilia mkazo kwa
wageni wanaoingia nchini. Kwa namna hiyo juhudi zitafanyika kuhakikisha wageni
wote wanapimwa kabla ya kushiriki michuano hiyo.
Baadhi ya wachezaji wageni ni pamoja na, Andrey Coutinho na Genilson Santana
‘Jaja’ (Yanga), Pierre Kwizera (Simba), Leonel Sant Prexue na Ismail Diara
(Azam) na wengineo.
Katibu wa chama cha wataalamu wa tiba (TASMA), Nassor Matuzya, amesema kuwa
hadi kufikia sasa hakuna hata timu moja ambayo imepeleka maombi kwaajili ya
kufanyiwa vipimo, jambo ambalo linaleta mashaka kwa shirikisho la soka la
Tanzania.