Kocha Mbrazil wa Yanga Marcio Maximo

Kufuatia kuzuka kwa wimbi la kuwepo kwa makocha na madaktari wasiokuwa na vigezo katika timu nyingi hapa nchini, SHIRIKISHO la soka la Tanzania limeamua
kuwafanyia uchunguzi makocha wa timu zote ambazo zitashiriki katika msimu wa soka wa ligi kuu mwezi ujao.

Kwa mujibu wa Ofisa wa Habari wa TFF, Boniface Wambura, amesema kuwa, wanazikumbusha klabu zote za ligi kuu na daraja la kwanza  kuwasilisha vyeti vya makocha wao pamoja na madaktari kabla ya ligi kuu kuanza ili waweze kuvikagua.

Miongoni mwa makocha wanaokusudiwa ni pamoja na makocha wa Simba, Mcroatia Zdravko Logarusic na Mbrazili wa Yanga, Marcio Maximo pamoja na wa timu zote za ligi kuu na daraja lakwanza.

Boniface Wambura amesema kuwa, TFF ina imani kuwa makocha wote wanasifa na vyeti vyao ambavyo vitawasilishwa mara moja kwaajili ya kufanyiwa ukaguzi. Kitendo hiki sio mara ya kwanza kufanywa na TFF bali ni kawaida.
 
Top