Mwanaume mmoja amekutwa na kuondolewa funza wapatao mia mojawalio hai tenawanaokula puani mwake na kuruhusiwa aende nyumbani.

Mwanaume huyo anatajwa kuwa na umri wa miaka sitini na mitano. Watabibu wanasema kuwa funza hao walikuwa wamejichimbia ndani zaidi ya pua yake.


Mwanamume huyo ni mwenye asili ya Sao Paulo, nchini Brazil,alikuwa akisumbuliwa mno na njia ya mfumo wa hewa hasa puani ,na pua yake ilikuwa imeathiriwa na mabuu ya inzi.

Pamoja na mambo mengine, mara kwa mara mwanaume huyo alikuwa akilalamika kuwa kuna minyoo pia huwa inadondoka kutoka puani mwake.

Tundu za pua ni mahali ambapo vijidudu virukavyo huweza kutaga mayai yao hapo na baadaye hugeuka kuwa funza.

Na wataalamu wa pua na koo wanasema kwamba chakula kikuu cha funza wakaao puani ni nyama za pua na endapo mgonjwa ataachwa bila kupatiwa matibabu ,funza hao wanauwezo wa kutafuna na kuharibu kabisa mfupa wa mwanzi wa pua,kuharibu vimishipa vya uso,pua na macho.

Na hali hiyo ikitokea,jua kutakuwa na maambukizi kwenye ubongo na macho na kwa kawaida husababisha ugonjwa wa uti wa mgongo na hata kifo.

Mwanaume huyo aliamua kwenda kwenye zahanati nchini Brazil kutoa malalamiko yake kwamba siku mbili nyuma aliona kitu kinachofanana na mnyoo ukichomoza na hatimaye kutoka katika pua yake upande wa kushoto.

Mwanaume huyo anaishi na virusi vya ukimwi ana tatizo la ini,na kinga yake ya mwili ilikuwa inapungua kwa kasi kubwa na alikuwa hajaanza kutumia vidonge vya kurefusha maisha.

Miaka mitano iliyopita alifanyiwa upasuaji wa pua yake baada ya kugundulika kuwa alikuwa na uvimbe puani na hakuona dalili yoyote hapo kabla,ingawa kwa wiki nzima kabla ya kuhudhuria zahanati alikuwa akitokwa na damu puani,maumivu ya pua upande wa kushoto Na harufu mbaya,alikuwa akishindwa kupumua sawa sawa na uvimbe ulianza kuonekana usoni na puani mwake.


Lakini baada ya kudumbukiza kijikamera kidogo puani mwake ,aligundulika
Madaktari wakaanza kuwatoa funza hao kwa muongozo wa kamera iliyokuwa ikiangaza puani na kuitibu pua yake.

Iliwachukua siku nne madaktari kuondoa uambukizo katika pua ya mwanaume huyo na baada ya hapo madhila yake yakakoma na baada ya uangalizi wa mwisho kwa kutumia kamera ile ile imethibitika kwamba tatizo lake lime kwisha.
 
Top