Watu
10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa msikitini wakiwa
na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la
wapiganaji wa Al Shabaab wa nchini Somalia.
Baadhi ya fifaa walivyokamatwa navyo watuhumiwa.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonald Paul
alisema tukio hilo limetokea jana (Aprili 14 mwaka huu) majira ya saa 3.30
usiku katika kitongoji cha Nyandero, tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero.
Aidha
alisema siku ya tukio polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watu
hao na kwamba walitaarifiwa kuwa wanajihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu
na polisi waliamua kufatilia nyendo zao.
Kamanda
huyo alisema walianza kuwasaka watu ambao walipata taarifa wapo katika Msikiti
wa Suni uliopo Kidatu.
“Polisi
walipofika katika msikiti huo waliuomba uongozi wa msikiti huo kuwatoa watu
wote waliokuwa msikitini ili kuweza kubaini watu ambao wanatiliwa mashaka,”
Alisema
polisi waliendelea na ukaguzi na kuwakamata watu hao 10 wakiwa na vifaa hivyo
na kuwatia nguvuni.