Idadi kubwa ya watu wanao jitoa uhai wao wenyewe katika jamii ni wanaume kuliko wanawake. Jambo hili limepelekea wataalamu kulifanyia uchunguzi ili kuweza kubaini ni sababu gani ambazo zinapelekea matukio kama hayo kuwakuta wanaume zaidi kuliko wanawake.
''Miaka 40 ni miaka ambayo mtu ana majukumu
mengi, Unaweza kudhani kuwa mke wake amemuacha na kuchukua watoto wote,au
kapoteza kazi yake katika umri huo wakati ni vigumu kupata mwingine''alihoji
Jack.
''Au sababu yoyote ambayo inaweza kumpa shinikizo
mwanaume ambaye anahitajika kuhudumia familia yake''.
Kila mtu atakubali kuwa ni tatizo kubwa katika
familia pale unapompoteza mtu kwa sababu ya ugumu wa maisha uliokithiri au
kuachwa na mpendwa wako.
Wengine walitoa maoni kuwa wengi wanaojiua ni ushahidi
tosha kuwa wana matatizo ya kiakili au wana msongo wa mawazo au huzuni katika
maisha.
Prof Rory O'Connor ambaye anaongoza kituo maarufu
duniani cha utafiti katika chuo kikuu cha Glasgow, anasema tabia ya kujuiua ni tatizo la
kisaikolojia ambalo hutokana na upungufu wa kiakili.