Mtoto mmoja wa miaka minane amesafirishwa hadi nchini uhispania kutoka Moroco akiwa ndani ya sanduku kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Uhispania
Wakati polisi walipolifungua sanduku hilo, mvulana huyo alikuwa katika hali
mbaya sana.Mvulana huyo kutoka Ivory Coast sasa anahudumiwa na mamlaka ya
Cueta.
Gazeti la Uhispania El Paris liliripoti kwamba msichana huyo wa miaka 19
hana uhusiano na mtoto huyo na kwamba alilipwa na babaake ili kubeba sanduku
hilo.
Babaake mtoto huyo anaishi katika visiwa vya Conary na kwamba alitarajia
kuonana na mwanawe kulingana na gazeti hilo.
Chombo cha habari cha Uhispania Efe kimesema kuwa babaake mvulana huyo
ambaye anajulikana kama Abou alisafiri hadi nchini Ivory Coast kumchukua
mwanawe baada ya kuhamia katika eneo la Gran Canaria mwaka 2013.
Babaake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye
alimsafirisha mtoto huyo kupitia sanduku.
Msemaji wa polisi aliiambia Efe:''Alionekana kusita na kama ambaye hakutaka
kupitia mpakani''.
Chanzo BBC