Magazeti nchini India yameripoti kisa cha kutamausha kilichotokea katika ndege ya shirika la Air India.
Abiria
mmoja aliyekuwa safarini kuelekea mjini London Uingereza akitumia ndege
ya shirika la ndege ya Air India alizua hofu miongoni mwa abiria
wengine alipopiga kamsa kwa mshtuko baada ya kumpata mjusi kafiri ndani
ya mlo wake.
Abiria wote walitamauka wasijue kilichompata mwenzao
haswa wakati huu ambapo kunataharuki kubwa na tahadhari kuhusiana na
maswala ya usalama kufuatia matukio ya ugaidi kote duniani.
Mjusi kwenye mkate
Bwana
huyo ambaye awali alikuwa ameagiza chakula maalum kutoka kwa mhudumu wa
ndege hakuamini macho yake alipokaribia kumla mjusi macho makavu !
Inasemekana kuwa alipofungua mkate wake akitaka kuunga'ta mara akaona ukitikisika. Ghafla bin vu akaona mjusi akijifurukuta akitafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye plastiki iliyokuwa imefunika chakula chake.
Alipiga mayowe kwa sauti ya juu usingeliamini kuwa ni mwanaume.
Shirika
hilo limekanusha habari hiyo japo kuna picha inayoendelea kusambazwa
katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikionesha mjusi mdogo
kwenye mkate.
Waziri wa usafiri wa anga ametao onyo kwa shirika hilo akisema kuwa halifai kuwapakulia wateja wake mijusi!
Chanzo: BBC