Watanzania Wenzangu,
Leo Tarehe 29 October 2015, kwa kupitia Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma Duni Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa
2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Tumeainisha
kwenye malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio
mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi
yaliyopatikana kwenye vituo vya kupiga kura, kama ifuatavyo.
•
Upunguzwaji wa kura zangu
•
Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
•Tunaendelea
kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa
kwa Demokrasia kunakooneka wazi kutokana na mwenendo wa Tume kuendelea
kutangaza matokeo ya kura yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi wetu.
Aidha,
kumekuwepo pia na uporaji wa ushindi kwa wagombea wa vyama vya UKAWA kwenye
ngazi ya Ubunge na Udiwani
Kama
tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza kwa
zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa
na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za
matokeo nchi nzima.
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Naendelea
kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua, MImi, pamoja na
viongozi wenzangu tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja Amani, lakini
sote tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata
mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji, hivyo nitaendelea kuwa pamoja na
watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote.
Tanzania
kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha amani katika Afrika, tunashangaa
leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha
za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita, hii ni kuwatisha wananchi ili
wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka,
nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo.
Lowassa,
Edward Ngoyai