Basi moja lililokuwa likisafiri kutoka mjini Juba kuelekea Kampala Uganda limevamiwa na kufyatuliwa risasi asubuhi ya siku ya Alhamisi.
Kulingana na Mwandishi mmoja katika eneo hilo Philip
Thon,kisa hicho kilitokea mwendo wa saa moja katika eneo la Moli yapata
kilomita 50 kutoka mji wa mpakani wa Nimule.
Maafisa wa Polisi wa Sudan Kusini wanajaribu kutafuta idadi
kamili ya watu waliojeruhiwa.
Watu wanne waliofariki na wengine wanne waliojeruhiwa
wamepelekwa katika hospitali ya Juba.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa huenda takriban watu 25
wameuwawa huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.
Chanzo chetu mjini Kampala kimezungumza
na kamanda wa polisi wa jimbo la Kaskazini mwa Uganda ,karibu na mpaka na Sudan
Kusini.
Amesema kuwa maafisa wake wanakutana na kujadiliana na wenzao
wa Uganda ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Amesema kuwa wanajaribu kutafuta njia ya kuwasafirisha
waliojeruhiwa katika hospitali ya Lacor huko Gulu nchini Uganda.
Amekadiria kwamba takriban watu 69 walikuwa wakiabiri basi
hilo.
Patience kwa sasa anajaribu kuitafuta kampuni ya basi hilo
kwa jina Friendship.
Haijabainika ni nani aliyeshambulia lakini baadhi ya
waliojeruhiwa ambao walizungumza na waandishi ,wanasema washambuliaji walikuwa
wamevalia sare za jeshi la Sudan Kusini na walikuwa wakizungumza lugha ya eneo
hilo.
Biashara imenoga kati ya Kampala na Juba ambapo mabasi na
malori yanatumia barabara hiyo.
Ni mara ya kwanza kwa basi la abiria linalotumia barabara
hiyo kuvamiwa katika kipindi cha siku za hivi karibuni