Katika hali isiyo ya kawaida mtoto mmoja aliye julikana kwa majina ya Elena Mussa mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitano mkazi wa kijiji cha Mazoka wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro amekutwa akiwaamekufa ndani ya kisima cha maji kwa kile kilicho daiwa kudumbukizwa na baba yake mzazi mwenye matatizo ya akili kwa muda mrefu.
Wakizungumza na ITV mashuhuda wa tukio hilo na ndugu wa marehemu wamesema wakati walipo enda kuchota maji katika kisima hicho waliuona mwili wa mtoto huyo ukielea majini kisha kutoa tarifa kwa mwenyekiti wa kijiji.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Rozi amesema baada ya kuona tukio hilo alitoa tarifa Polisi ndipo taratibu za kutoa mwili huo zilianza huku babu wa marehemu Bwana.Mwanangumi Makala akieleza jinsi kifo cha mjukuu wake kilivyo tokea.
Kwaupande wake mganga wa Hospital ya wilaya ya Kilosa Julius Chiduo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo akitoa taarifa za uchunguzi wa mwili wa marehemu amesema mtoto huyo amefariki baada ya kukosa hewa kwa kuzibwa pua na kushindwa kupumua jambo ambalo limepelekea kupoteza uhai wake.