MCHINA MAUAJI GEITA (1)
Mr. Swii akimshushia kipigo kijana Elisha adi kukatisha uhai wake.

Kijana mmoja aliyejukikana kwa jina moja (Elisha) mkazi wa Kabindi Mkoani Geita amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa na raia wa China aliyefahamika kwa jina la “Mr. Swii” kwa madai ya kwamba alilalamika ili wapandishiwe ongezeko la mshahara. Taarifa zinadai waliopigwa wengine wawili wako hospitali kwa matibabu zaidi.

 Inasemekana baada ya Elisha kupigwa na Mchina huyo, alienda hospitali ili akapatiwe matibabui kwa maana alikuwa na hali mbaya, bada ya tiba ya awali hapo aliambiwa arudi kazini huku hali yake ikiwa mbaya na ndipo alipodondoka na kuzimia. Wakafanya jitihada ya kumpeleka Hospitali ya Mkoa kabla ya kufariki dunia.
 Tukio hilo la kikatili limetokea katika Mgodi wa Nyamahuna uliopo Katoro Mkoa wa Geita. Mgodi ambao ni maaufu kwa uchimbaji wa dhahabu na shaba.
Mashuhuda wanasema kuwa “Mr. Swii” pamoja na walinzi wa Mgodi huo ndio waliohusika katika kuwapiga Wafanyakazi hao na kupelekea mfanyakazi mmoja kufariki Dunia kwa Kipigo hicho.

 https://www.googleadservices.com/pagead/aclk?sa=L&ai=CelEIy-yNV-CrOPCHzAap7IWIAsuf5JtFmJajj8UDwI23ARABINq1kCNgw4aiBqABmPWSswPIAQmpAkAN6s13E7E-qAMByANAqgSKAU_QYVchY5LGOtz2s3tQ-05MF1Vom_PQidbjAVdnEl4vBL4cRBltQZexlcyGqXtEHeNbQ0Mc8C_oG1-DhyTEc30y59KreMMzefBFltbzo60_H2uyMj-3imVARsKZnoeZ2c-0FvIm7_89fIoYdBbmXlo6jGk6eKGyu6DJX0EaXaJWU-dP6Yt-BGgiXIgGAaAGLoAH0IrtTKgHpr4b2AcA2BMM&num=1&cid=CAASEuRoY0qBl--4c_L0h7k1DiHFBg&sig=AOD64_23wpVwNsisKGhDriBQmOFcESneIg&client=ca-pub-8314364456781507&adurl=https://tender.singles/en%3Fcp%3Dted%26ag%3D33601067488%26ad%3D121484556688%26ti%3Dkwd-0%26tg%3D%26pl%3Dnewzatza.blogspot.com%26ap%3Dnone%26kw%3D%26mt%3D

MATUKIO ZAIDI YA KUSISIMUA BOFYA HAPA
 
Top