Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuachia madaraka kushindwa kusimamia suala la mchanga wa dhahabu unaosafirishwa kwenye makontena.
Amemtaka waziri huyo kujitathimini na bila kuchukua muda mrefu aachie madaraka kutokana na suala hilo.
Rais Magufuli amesema hayo baada ya kamati iliyokuwa ikichunguza suala la mchanga kwenye makontena kukabidhi ripoti yao.
Kamati hiyo ya wataalamu wa jiolojia na uchambuzi wa kisayansi iliyoundwa Machi 29 mwaka huu, ilichunguza aina ya madini yaliyopo, kiasi na viwango vya ubora.
Akikabidhi ripoti hiyo, Profesa Mruma amesema uchunguzi huo umebaini uwepo wa madini ya kiasi cha kati ya Sh829.4 bilioni mpaka 1.439 Trillion kwa makontena yote 277.
"Licha ya uchunguzi uliofanywa kupitia makontena haya, tumegundua uwepo wa aina nyingi zaidi za madini ambayo hayakuwa yakijulikana na haya yamekutwa na thamani ya kati Sh129.5 bilioni mpaka261 bilioni," amesema Profesa Mruma.



    TANGAZO 
 
Top