Mtu mmoja Mkoani Katavi anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga kwa shoka mke wake na kumsababishia kifo kisha kumfungia ndani.
Chanzo cha habari hii kimesema kuwa Marehemu Benaderta (38) kabla ya kifo chake alikuwa akiishi na mume wake huyo pamoja na watoto wao wawili, hata hivyo mume wake huyo alikuwa na kawaida ya kumpiga mara kwa mara.
Majirani wa Benaderta ambao ni Antony na Mayanga ndio waliobaini kufanyika kwa unyama huwo pale walipokuwa wakipita njia karibu na nyumba ya Mareheu wakielekea shambani, walibaini hali ya utofauti katika nyumba hiyo.
Majirani hao walikwenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji kisha wakaenda kwa Mtendaji wa kijiji na baada ya hapo wakaelekea eneo la tukio.
Walikuta mlango wa nyumba hiyo umefungwa kwa nje kwa kutumia kamba jambo lililoashiria kuwa ndani hapakuwepo na mtu. Waligonga mlango huwo kwa muda bila kuitikiwa na mtu ndipo walipochukua jukumu la kuvunja mlango na kuingia ndani.
Walimkuta marehemu akiwa tayari amekwisha kufariki na walipomchunguza wakabaini kuwa kifo chake kilikuwa kimesababishwa na kupigwa kwa kitu kizito kinachoelekea kufanana na shoka ama nyundo kubwa kwenye kichwa chake.
Hata hivyo hawakukuta mtu mwingine ndani humo, watoto pamoja na mume wake huyo haifahamiki wapo wapi. Hivyo jeshi la polisi linamsaka mtu huyo kwa tuhuma za mauaji