Mwanamke
 mmoja aliyefahamika kwa jina la Magdalena Limano (32) mkoani Iringa 
anashikiliwa na polisi baada ya kujifungua mtoto na kumtumbukiza chooni.
Kwa
 mujibu wa chanzo cha habari hii, Magdalena alimzaa mtoto huyo tarehe 4 
na kumtumbukiza chooni kwa lengo la kumuua, hata hivyo Mungu si  
Athumani wala si Fatuma, kwani asubuhi ya Tarehe 5 majirani walisikia 
sauti ya mtoto huyo ikilia kwa masikitiko kutokea chooni.
Majirani waliosikia sauti ya mtoto huyo walitoa taarifa na punde wakashirikiana kuvunja choo na kumtoa kiumbe huyo aliyekuwa amehukumiwa pasipo kuwa na hatia masikini ya Mungu.
Mtoto Mchanga baada ya Kuokolewa kutoka kwenye shimo la choo
Kwa
 mujibu wa maelezo ya Majirani wa Magdalena, walisema kuwa mama huyo 
alifanya kitendo hicho ili kumficha mume wake aliyekuwa safarini 
asifahamu kama alipata ujauzito kwa mwanaume mwingine na kujifungua.
Walimalizia
 kwa kueleza kuwa, ni kawaida ya magdalena kumsaliti mume wake kila 
anapokuwa safarini kwa kutemba na wanaume wengine (michepuko).
Katika
 ulimwengu huu hakuna anayepanga mauti ya mwingine labda kama Mungu 
apende, Kichanga huyo aliyeokolewa kutoka kwenye dimbwi la kinyesi  anaendelea vizuri akiwa hospitali na Magdalena anashikiliwa na jeshi la polisi kwaajili ya kujibu shitaka.
Bofya Hapa kupitia matukio zaidi ya Kusisimua>>


