Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Magdalena Limano (32) mkoani Iringa anashikiliwa na polisi baada ya kujifungua mtoto na kumtumbukiza chooni.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii, Magdalena alimzaa mtoto huyo tarehe 4 na kumtumbukiza chooni kwa lengo la kumuua, hata hivyo Mungu si  Athumani wala si Fatuma, kwani asubuhi ya Tarehe 5 majirani walisikia sauti ya mtoto huyo ikilia kwa masikitiko kutokea chooni.

  
Majirani wakiwa Eneo la Tukio

Majirani waliosikia sauti ya mtoto huyo walitoa taarifa na punde wakashirikiana kuvunja choo na kumtoa kiumbe huyo aliyekuwa amehukumiwa pasipo kuwa na hatia masikini ya Mungu.
 
Wasamaria wema wakifanya jitihada za kumuokoa mtoto aliyetupwa chooni na mama yake

Kwa mujibu wa maelezo ya Majirani wa Magdalena, walisema kuwa mama huyo alifanya kitendo hicho ili kumficha mume wake aliyekuwa safarini asifahamu kama alipata ujauzito kwa mwanaume mwingine na kujifungua.

Walimalizia kwa kueleza kuwa, ni kawaida ya magdalena kumsaliti mume wake kila anapokuwa safarini kwa kutemba na wanaume wengine (michepuko).

Katika ulimwengu huu hakuna anayepanga mauti ya mwingine labda kama Mungu apende, Kichanga huyo aliyeokolewa kutoka kwenye dimbwi la kinyesi  anaendelea vizuri akiwa hospitali na Magdalena anashikiliwa na jeshi la polisi kwaajili ya kujibu shitaka.
                   
   Bofya hapa Kupitia Matukio ya Kusisimua Hapa>>             

 
Top