SIMULIZI YA KUSISIMUA Sehemu ya Tano (5)
Ilipoishia...
“Hivi yule chokoraa uliyeingia naye yuko wapi?” Suzy alihoji kwa msisitizo huku akiwa haelewi chokoraa aliyekuwa anamzungumza ndiye yule kijana mzuri aliyetambulishwa na mama yake.
“Hivi yule chokoraa uliyeingia naye yuko wapi?” Suzy alihoji kwa msisitizo huku akiwa haelewi chokoraa aliyekuwa anamzungumza ndiye yule kijana mzuri aliyetambulishwa na mama yake.
Endelea…
“Suzy, mtu niliyeingia naye ni kaka yako Ayubu, na sio chokoraa”
“Haaa!”
“Kwani vipi?”
“Naomba unisamehe kaka Ayubu” Suzy alimuomba msamaha Ayubu kwa yote
aliyomfanyia wakati alipokuwa anafika. Hakuamini kama yule mtu mchafu angeweza
kuoga na kupendeza kiasi kile. Ayubu alimwambia Suzy kuwa alikwisha kumsamehe.
Suzy alitoka nje na kwenda kuendelea na usafi wa nguo zake
****
Baada
ya miezi miwili tangu Ayubu kufika pale nyumbani kwa Mama Suzy alikuwa
amebadilika kwa kiasi kikubwa. Alikuwa amenawiri na kupendeza sana .Alikuwa
amekwisha sahau matatizo yote ambayo alikumbana nayo wakati anaingia jijini.
Alikuwa amekwisha kata tamaa ya kumtafuta rafiki yake Kondo kwasababu hadi muda
ule hakuwa amemuona wala kusikia habari zake.
Tabia yake nzuri ndiyo ilikuwa silaha kubwa katika maisha yake pale nyumbani
kwa Mama Suzy. Mama Suzy alikuwa ni mama yake na mzee Manyama alikuwa ni baba
yake. Hivyo Ayubu aliishi kama mtoto wa familia ile. Mzee Manyama alimtafutia
shule kijana wake ili aendelee na masomo ya sekondari. Hivyo Suzy na Ayubu
wakawa wanasoma kidato kimoja lakini shule tofauti.
Waswahili wanasema kuwa “ukila muwa huwezi kukosa fundo.” Suzy alikuwa ni
tatizo katika maisha ya Ayubu. Mara kadhaa alikuwa akimtia majaribuni lakini
Ayubu alikuwa akimuomba sana mungu amuepushie balaa lile. Alikuwa akiwaheshimu
sana wazazi wake, hivyo alifahamu kuwa kama ange fanya mzaha angejiharibia
mwenyewe.
Siku moja Ayubu na Suzy walikuwa mezani wakijisomea. Wakati huwo wazazi wao
walikuwa wamela chumbani. Suzy alitumia muda mwingi kumuangalia Ayubu kuliko
kusoma. Ayubu aliligundua jambo lile na kujikuta akihoji.
“Vipi dada Suzy, mbona husomi?”
“Aah! Nasikia baridi” alijibu Suzy kwa sauti iliyotokea puani.
“Nenda ukavae sweta” alisema Ayubu. Suzy aliinuka na kwenda chumbani. Alipotoka
alikuwa tofauti na vile alivyo fikiria Ayubu. Suzy alikwenda kubadilisha nguo
na kuvaa kimini kilichoshindwa kuyaficha mapaja yake. Juu alikuwa amevaa blauzi
isiyokuwa na mikono ambayo nayo ilikuwa wazi maeneo ya kifuani na kupelekea
nusu ya matiti yake kuonekana. Alipofika karibu na Ayubu alidondosha kalamu,
aligeuka na kuiokota huku sehemu za makalio zikiwa kwa upande wa Ayubu. Kitendo
kile kilipelekea blauzi aliyokuwa amevaa kupanda juu na kuonesha nguo yake ya
ndani.
Ayubu alipomuona Suzy alijikuta mwili wake ukimsisimka. Ayubu alimtazama
kuanzia chini hadi juu na kumthaminisha ndani ya sekunde kadhaa. Kiukweli Suzy
alikuwa ameumbwa vilivyo. Kumbe uzuri wa miguu yake haukuishia nje. Mapaja
meupe yaliyo ungana na mlima wa makalio yake yalitosha kumpagawisha mwanaume
yeyote aliyekuwa rijali. Kiuno chake kilichokuwa kimepambwa kwa rastiki
ya nguo yake nyeupe ya ndani kilikuwa ni cha pekee.
Ayubu alimeza funda la mate kisha kwa haraka sana kabla Suzy hajainuka
alirudisha macho kwenye kitabu alichokuwa anasoma. Moyoni mwake alijisemea kuwa
endapo Suzy asingekuwa dada yake asingekubali kumuacha. Suzy alipofika mezani
hakwenda kukaa kwenye kiti chake, alisimama pembeni ya Ayubu kwa mapozi. Loo!
Ayubu alipoinua macho kumtazama Suzy akaona mabo yanazidi kumuwia magumu.
Sehemu kubwa ya chuchu zake zilizo chongoka kama sindano zilikuwa wazi. Ayubu
akakwepesha macho yake na kuangalia pembeni.
“Sasa dada Suzy ulisema unasikia baridi, inakuwaje tena umevaa hivyo?” Ayubu
alihoji kwa upole. Suzy alimtazama kisha akatingisha kichwa.
“Inamaana wewe ni mtoto ndogo?” Suzy alihoji huku akibinua midomo.
“Kwanini unasema hivyo dada Suzy?”
“Ayubu….” Suzy aliita kwa sauti ya kutokea puani.
“Nakusikiliza Suzy”
“Kusoma hujui lakini hata picha pia huoni?”
“Unamaanisha nini?” Ayubu alihoji swali ambalo lilionekana kumkera Suzy. Suzy
alikunja uso na kutoa msonyo mrefu kisha akaenda kuketi kwenye kiti chake.
Alipofika alishika kichwa kwa mikono yake miwili badala ya kusoma. Ingawa Ayubu
alikwisha fahamu kitu alichokuwa akikitaka Suzy lakini akawa anajifanya
haelewi. Alimtupia jicho la wizi mara kwa mara na kumkuta bado alikuwa
amejiinamia.
“Unaumwa Suzy” Ayubu alitupa swali la kizushi. Suzy aliinua sura na kumtazama
Ayubu kwa hasira kisha akaachia tena msonyo na kuinuka kuelekea chumbani kwake.
Ayubu alifahamu kuwa Susi alikuwa amekwenda kulala. Alitingisha kichwa
kumsikitikia kisha akaendelea kusongoka. Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Suzy na
Ayubu pale nyumbani kwa mama Suzy.
****
Mzee
Manyama alikuwa amesafiri kikazi kwenda mkoani Singida. Mama Suzy naye
alipata taarifa za kufiwa na mjomba wake aliyekuwa akiishi Mtwara. Kutokana na
hali hiyo ilibidi Suzy abaki na kaka yake Ayubu. Mama Suzy aliwasisitizia
wanawe waishi vizuri pindi watakapo bakia wawili. Moyo wa Suzy ulijawa na
furaha kubwa kwa kitendo cha wao kubaki wawili tu nyumbani. Aliamini kuwa ni
lazima angekipata kile alichokitafuta kwa muda mrefu kutoka kwa Ayubu.
Siku moja Ayubu alikuwa ameketi sebleni akitazama runinga mara baada ya kutoka
shule. Suzy alifika akiwa amevalia nguo za kumtega kama ilivyokuwa kawaida
yake. Alikwenda kuketi kwenye kochi la mbele ambalo ni lazima Ayubu
angemwangalia. Sketi yake fupi ilipanda juu na kusababisha nguo yake nyeupe ya
ndani kuonekana. Ayubu alimtupia jicho lakini alivyokutana na hali ile
aliyarudisha macho yake kwenye runinga. Kisha akamuomba mungu kimoyomoyo
amsaidie kuepuka matatizo yale.
Suzy
alipoona kuwa mtu aliyekuwa akimtega hakuwa na muda wa kumuangalia ilimbidi
alazimishe.
“Ayubu….” Aliita Suzy kwa sauti ya mahaba.
“Naam” Ayubu aliitika huku macho yakiwa kwenye runinga.
“Yaani nakuita hutaki kuniangalia?”
“Ah! Samahani dada Suzy” Ayubu alijifanya kuhamaki na kumuangalia Suzy.
Alipomwangalia kifuani matiti yalikuwa wazi kwa kiasi kikubwa, chini ndio kila
kitu kilikuwa wazi. Akaamua kumtazama machoni pasipo kupanda wala kushuka. Hata
hivyo Suzy alionekana kukosa cha kuzungumza. Aliweka kidole mdomoni na kurembua
macho. Loo! kumbe Suzy alikuwa amebarikiwa macho. Ayubu alijikuta akishindwa
kumtazama na kupepesa macho kuangalia pembeni.
“Vipi mbona huongei sasa?” alihoji Ayubu.
“Unadhani nitaongea nini?”
“Siwezi kujua”
“Aaaah!” Suzy alihamaki kama vile alikuwa amechomwa na mwiba. Alijiinua pale
alipokuwa ameketi na kukimbilia alipokuwa amekaa Ayubu. Alijifunua mgongoni
huku akilia.
“Hembu niangalie hapa kuna mdudu amening’ata” alisema Suzy akiwa ameketi
pembeni mwa Ayubu.
“Vipi dada Suzy una nini?” Ayubu alihamaki huku akikagua pale alipokuwa
akioneshwa na Suzy. Mnh! Ayubu alishuhudia mzigo wa shanga kiunoni mwa Suzy.
Alivuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu. Alijifanya hakuziona zile shanga na
kumuuliza mahali palipokuwa pakimuwasha.
“Mbona sioni kitu” Ayubu alihoji huku macho yakiwa kwenye zile shanga.
“Hapo…..shuka chini…tena….aah! hapo hapo” Suzy alikuwa akimuelekeza Ayubu ili
aone zile shanga zake, kumbe Ayubu mwenyewe alikuwa amekwisha kuziona mapema
sana.
“Hakuna mdudu. Labda awe amekimbia” alisema Ayubu na kutaka kuondoa mkono wake.
“Aaah!...No!...usitoe mkono. Naomba nikune pananiwasha” alisihi Suzy. Ayubu
ilimbidi afanye kile alichoagizwa na Suzy. Wakati Ayubu akimkuna Suzy alianza
kutoa sauti na miguno ya mahaba.
“Aaah!.... yeah!.....Oooh!..hapo hapo….Sweety….Mmm….tamu” alilalamika Suzy kwa
sauti ya chumbani huku akijilegeza na kujikuta akitaka kumlalalia Ayubu.
Ndugu msomaji wetu, tupo tayari kukupa taarifa kila tunapotoa toleo jipya la simulizi hii ya kusisimua. kitu cha kufanya LIKE ukurasa wetu wa Facebook hapa >> Bofya hapa