Sailson das Gracas amekiri
kufanya mauaji hayo kwa sababu anasema alipenda kufanya hivyo
Polisi wanasema walimkamata Sailson Jose das Gracas mnamo siku ya Jumatano, baada
ya kumdunga kisu mwanamke ambaye alifariki muda mfupi baadaye.
Alikiri kuwaua wanawake wengine 37 , wanaume watatu na mtoto mdogo wa miaka
2.
Polisi wanasema wanawasaka waathiriwa na kusema wameweza kuwapata watu
wanne.
Katika mahojiano na vyombo vya habari, polisi walisema kua mwanamume huyo
kawaida alikuwa anaondoka kwake na kuwawatufuta waathiriwa lengo lake likiwa ni
kuua 'kwa raha zake.'
Aliambia polisi kuwa wakati atakapoondoka gerezani hatasita kuua tena.
Alisema kuwa alipendelea kuwaua wanawake wazungu ambao aliwanyonga.
Wanaume watatu ambao aliwaua, alifanya hivyo alipokodiwa kama mamluki.Endelea>>