Wizara ya Maliasili na Utalii imekamata kontena 31 yenye magogo aina ya mitiki katika Bandari ya Dar es Salaam yaliyodaiwa kupatikana kwa njia ya wizi na kutaka kusafirishwa nje ya nchi kinyume na Sheria ya Misitu ya mwaka 2002 inayozuia kusafirisha magogo yasiyo ongezwa samani kwenda nje ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Adelhelm Meru amewambia waandishi wa habari wakati alipofanya upekuzi wa makontena baada ya kupata taarifa na kukua magogo hayo yalikuwa yamefikishwa bandari hapo kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kinyume na sheria.
Amesema Wizara yake kwa kutumia vyombo vyake vya upelelezi vilivyopo kwenye mamlaka na wakala wa Misitu Tanzania iliweza kupatiwa habari kuna makontena yenye magogo bandari yanasafirishwa nje ya nchi na kufika bandari hapo haraka kujionea.
Uchunguzi unaofanyika utatupatia suluhisho mwishoni na namna ya kupambana na uharifu kama huu na Afrika kwa pamoja tunahitaji kushirikiana badala ya kujiibia wenyewe na kwenda kuyatajirisha mataifa mengine nje ya Afrika.
Magogo haya sasa yapo hapa Tanzania na haijathibitishwa kuwa yanatoka Zambia uchunguzi unaendelea ili kujua wahusika wa huu mzigo na kuchukuliwa hatua za kisheria kwani ni makosa kusafirisha magogo yasiyoongeza thamani.
Chanzo: ChanelTen