Tukio la kushangaza linaendelea kuwaduwaza watu baada ya mtoto Irene Joseph (1) mkazi wa Kibamba jijini Dar es salaam Kufariki mwezi Agost mwaka jana akiwa na umri wa miezi 9 na kufufuka hivi karibuni akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi minne.
Chanzo cha habari hii kimeeleza kuwa mama wa mtoto huyo Hellena Raphael na mume wake Emanuel Joseph walimpoteza mtoto wao kipenzi baada ya kufariki dunia kutokana na ugonjwa uliompata ghafla ambao ulifanana na degedege.
Mama mzazi wa Irene ameeleza kuwa baada ya kifo cha mtoto wake huyo, alipata taarifa kutoka kwa mchungaji wa kanisa Salala Nabii Flora kuwa mtoto wake alikuwa hai. Mchungaji huyo alimueleza kuwa mtoto Irene alikuwepo hai lakini kwa nguvu za mchungaji huyo asingeweza kumfufua.
Helena Raphael mama wa mtoto Irene
"Kuna dada mmoja pale kanisani alimsikia mchungaji Flora akiniambia hivyo ndipo akaniita pembeni na kunieleza kuwa Dodoma kuna mganga mwenye uwezo wa kurudisha watu waliokufa kimazingara, akanipa namba zake nikamwambia mume wangu na kuanza kuwasiliana naye" alisema Helena.
Baada ya kuwasiliana na mganga huyo aliwaambia washike shilingi mia moja mkononi na hapo ndipo alipowafahamisha kuwa ni kweli mtoto wao alikuwa hai. Walimpatia kiasi cha pesa alichokitaka na baada ya siku kadhaa mganga aliwafahamisha kuwa waende Dodoma kwani mtoto wao alikuwa tayari amepatikana.
Mwezi Februari mwaka huu Hellena na mume wake walisafiri hadi dodoma kwa mganga na kweli wakamkuta mtoto wao akiwa hai lakini mwenye afya dhoofu. Hivyo mganga aliwataka wamuache ili apatiwe matibabu zaidi.
Baada ya miezi miwili mganga alifika Dar akiwa na mtoto Irene akiwa mzima kabisa na mwenye afya nzuri.
Majirani wa Helena walikiri kuwa mtoto huyo alikuwa ni yuleyule Irene pamoja na kwamba ni mwaka umepita tangu alipofariki.
Kaburi alilozikwa mtoto Irene Raphael
Mjumbe wa mtaa huo Maimuna Abdala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake na pia amethibitisha kuwa mtoto huyo ni kweli alifariki na kuzikwa mwaka jana mwezi Agost na kufufuka mwaka huu 2015.
MATUKIO YA KUSISIMUA ZAIDI BOFYA HAPA>>