Mzozo mkubwa umezuka katika kikao cha wanachama wa chama cha mapinduzi CCM na viongozi wa CCM kata ya Kimamba "A" kufuatia mgombea wa udiwani aliyeshinda kwenye kura za maoni kukatwa jina na wanachama kulazimishwa kurudia uchaguzi hali iliyosababisha kikao kuvunjika baada ya wajumbe kunyanyuliana viti na kutaka kupigana.
Chanzo chetu kimeshuhudia wanachama hao wakiongea kwa jazba huku wengine wakinyanyua viti kupinga kitendo cha kurudia uchaguzi kwa mara ya pili nakusema endapo watalazimishwa watakihama chama hicho na kwenda vyama vya upinzani ambapo kikao kilivunjika na wajumbe wakaanza mzozo na mambo yalikuwa hivi.

Aidha wanachama hao wameitaka viongozi CCM wilaya kutovuruga matokeo hayo nakumtangaza aliyeshinda na vinginevyo wachague mwingine kati ya watu watano waliogombea huku mwenyekiti wa kata Mussa Guzungwa ambae ndiye aliyeshinda kura za maoni kugombea udiwani akijiuzulu na kuhamia vyama vya upinzani.


Naye katibu wa CCM kata ya Kimamba “A” Samweli Warioba amesema tarifa hizo za malalamiko ya wanachama wamezipeleka kwa viongozi wa CCM wilaya ya Kilosa na kwamba hawakubaliana na maamuzi ya kurudia uchaguzi.
Chanzo ITV
 
Top