Ndugu waandishi wa Habar, Tumewaita hapa muwaeleze watanzania wenzetu, Jumuia ya kimataifa na marafiki zetu wengine wa ndani na nje, kwamba hatukubaliani na mtokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais, yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kote nchini. 

Hii ni kwa sababu, upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa matokeo hayo umevurugwa kwa makusudi na watendaji ndani ya NEC kwa kusaidiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Katika maeneo mengi ambako matokeo yameshatangazwa mpaka sasa, kilichoripotiwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais, hakifanani wala kuendana na matakwa halisi ya wananchi. 

Matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli. 

Katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi, kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa mgombea wa CCM; maeneo mengine, kura zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya kura zilizopigwa. 

Kwa mfano, matokeo yaliyotangazwa na NEC katika majimbo ya Mkoani na Mtambile, kisiwani Pemba, Makunduchi, Kiwengwa, Donge, Tunduru, Tunduma, Same Mashariki, Chambani, Tandahimba, Kilindi na kwingi kwingineko, ni miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa hiki kinachotangazwa na NEC, siyo kura za uchaguzi mkuu wa rais. Tunaweza kuiita, “mzimu wa uchaguzi.” 

Ndugu waandishi wa habari; Tangu kuanza kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi huu, viongozi wetu wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) – mimi mwenyewe juzi na jana Mhe. Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Abdallah safari walilieleza kasoro zilizojitokeza katika matokeo ya rais,
 
Top