KIJANA mwenye umri wa miaka 25 aliyefahamika kwa jina la Makungu Kaneke, ameuawa kwa kuchomwa na mkuki akituhumiwa kuhusika na vitendo vya ushirikina.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema Kaneke amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Alisema aliuawa juzi alfajiri katika eneo la Ruviru na watu wasiojulikana akiwa amelala na mke wake aliyetajwa kuwa ni Bernadeta Kamahanga kijijini kwao Nyarugusu, Kata ya Heru Shingo wilayani Kasulu.
Alisema watu hao wanasaidiwa walimvizia na kumuua wakimtuhumu amekuwa akiwatesa wanakijiji wenzake kishirikina kwa muda mrefu.
Mpaka sasa, kwa mujibu wa Kamanda Mtui, hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kwamba upelelezi unaendelea ili watakaobainika wachukuliwa hatua za kisheria.
 
Top