Watu watatu wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti, katika wilaya za
Urambo Kaliua na Igunga Mkoani Tabora huku mmoja akikatwakatwa kwa kitu
chenye ncha kali, huku mwanamke akiuawa kwa fimbo na mmewe, na na mtoto
wa miaka tisa akifa kwa kupigwa radi akiwa anachunga mifugo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora Kamanda wa
Polisi Mkoani humo Kamishina Msaidizi Hamisi Suleimani, amekemea tabia
ya wafugaji ambao hawawapeleki watoto shule na kuwapeleka kuchunga
mifugo, jambo ambalo limesababisha kifo cha mtoto huyo.
Aidha katika hatua nyingine Kamanda Hamis Suleimani amewataka
wananchi Mkoani Tabora kuanzia tarehe 01/04/ mwaka huu 2016 wote
wanaomiliki silaha kama ni halali kuzisajili upya, na kama sihalali basi
watumie fursa hii kuzisalimisha maeneo yanayotambulika, na hapatakuwepo
na masharti ya aina