Mwanamke mmoja wa umri wa miaka 23 nchini India amekata uume ya wa kiongozi mmoja wa dini kwenye jimbo lililo kusini mwa nchi la Kerala, akidai kuwa alimbaka kwa miaka kadha.
Polisi wanasema kuwa kiongozi huyo wa dini kwa jina Gangeshananda Theerthapada, alikuwa akienda kwenye nyumba ya mwanamke huyo kufanya maombi kwa ajili ya afya ya babake.
Hii ni baada ya mamayake kuwa na matumaini kuwa mtu huyo ya Mungu angetatua matatiza ya familia yake.
Badala yake binti yake alidai kuwa alimdhulumu kingono kila mara.
Siku ya Ijumaa usiku alichukua kisu na kumshambulia wakati alijaribu kumbaka na kisha kuwaita polisi mwenyewe.
Mtuhumiwa huyo wa ubakaji kisha akakimbizwa hospitalini kwa matibabu ya dharura.
Hospitali hiyo ilisema mwanamume huyo wa miaka 54 kutoka Kollam alilazwa kwenye hospitali hiyo.
Uume wake ulikuwa umekatwa kwa asilimia 90 na hakuna uwezekano kuwa ungerudishwa tena..
Madaktari walijaribu kuzuia kufuja kwa damu na kumfanyia upasuaji ili aweze kupitisha mkojo.


 
Top