Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Pule Ntseki, amehukumiwa jela Kifungo cha maisha baada ya kukutwa na kosa la kumbaka bibi kikongwe mwenye miaka 77.


Kwamujibu wa chanzo cha habari hii, Pule Ntseki alifanya tukio hilo huko nchini Afrika Kusini ambako amemuingilia kwa lazima mwanamke mwenye umri wa miaka 72 ambaye alikuwa hajawahi kukutana na mwanaume kimwili.

Mwaka 2012, Pule alivunja nyumba ya Binti yatima mwenye umri wa miaka 14 na kumbaka. Kisha akatoweka pasipo kutiwa nguvuni.

'Siku za mwizi ni Arobaini, kwani bwana Pule alidakwa baada ya kumbaka bibi kikongwe ambaye ni bikira" kilieleza chanzo na kuendelea

"Mbakaji huyo alikutwa kwenye kitanda cha kikongwe huyo akiwa uchi wa mnyama (hana nguo)"

Baaba ya kukutwa ndipo mbegu zake za kiume zilipopimwa na kukutwa zinafanana na zile zilizokutwa kwa mtoto yatima aliyebakwa mwaka 2012. 

Mwanasheria Khuduga amesema kuwa, msichana aliyefanyiwa unyama huo amenyang'anywa haki yake ya elimu kwasababu tangu alipofanyia ukatili huo maendeleo yake ya darasani yalizidi kuporomoka siku hadi siku.

"Doctor aliyechukua vipimo vya mwanamke huyo kikongwe alibaini kuwa mwanamke huyo hakuwa amewahi kufanya mapenzi katika maisha yake (Bikira)

"Mahakama inapaswa kutoa adhabu kali ambayo itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizi. Hatukupendezwa kabisa na vitendo hivi vya kinyama" alisema Mateboho Lekatsa, mwananchi na kuendelea.
                      
   Pitia Matukio mengine hapa>>               


 


 
Top