Wabunge watano wamepewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya mkutano wa 20 wa bunge, kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge na kusababisha vurugu hali iliyopelekea Spika wa Bunge kuahirisha bunge.
Adhabu hiyo imetolewa na kamati ya haki maadili na madaraka ya bunge ambapo waliosimamishwa ni Mh Tundu Lissu, Mh John Mnyika, Moses Machali, Pauline Gekul na Mh Felix Mkosamali ambao hawataweza kuhudhuria vikao vya bunge hili hadi litakapovunjwa na wabunge wengine wawili Mh Peter Msigwa na Mh Rajab Mbarouck Mohamed wamezuiliwa kuingia vikao viwili vya bunge ambapo akisoma maamuzi hayo mjumbe wa kamati hiyo Mh Hassan Ngwilizi amesema.

Vurugu hizo zilitokea wakati waziri wa nishati na madini Mh Simba Chawene akiwasilisha muswada wa sheria ya petroli bungeni mjini Dodoma ambapo wabunge wa upinzani walianza kuomba muongozo wa spika huku Mh Chawene akiendelea kusoma muswada huo lakini baada ya muda alishindwa kuendelea baada ya kuzidiwa na kelele za wabunge hao hali iliyosababisha spika wa bunge Mh Anne Makinda kuahirisha bunge.

Mara baada ya kikao cha bunge kuahirishwa nje ya ukumbi wa bunge mbunge wa Ubungo Mh John Mnyika akazungumzia suala hilo kwa niaba ya wabunge wa kambi ya upinzani bungeni ambapo amesema kambi ya upinzania haiko tayari kuua ndoto za watanzania za kuondokana na umaskini kwa kutumia rasilimali zao na hapa anafafanua zaidi sababu za wao kupinga miswada hiyo.


Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh Jenista Mhagama amekanusha madai ya miswada hiyo kujadiliwa kwa siku moja na kudai kuwa ingeweza kujadiliwa hadi pale ambapo wabunge wangefikia muafaka na kuongeza kuwa ndiyo maana serikali iliamua isomwe mwishoni baada ya miswada mingine yote kujadiliwa.

MATUKIO YA KUSISIMUA ZAIDI BOFYA HAPA CHINI>>
 
Top