Hatimae Serikali imeondoa Mswada wa sheria ya upatikanaji habari wa mwaka 2015 bungeni ili kutoa fursa kwa wadau na kamati ya maendeleo ya jamii kuendelea kuujadili na kutoa maoni zaidi kwa lengo la kuboresha sheria.
Hatimae
serikali imeundoa mswada wa sheria ya upatikanaji habari wa mwaka 2015 bungeni
ili kutoa fursa kwa wadau na kamati ya maendeeo ya jamii kuendelea kuujadili na
kutoa maoni zaidi kwa lengo la kuboresha sheria hiyo.
Akitoa taarifa ya serikali bungeni,
waziri wa nchi ofisi ya rais asiye na wizara maalum, Prof Mark Mwandosya
amesema serikali imetafakari maoni ya kamati na kuafiki mswada uendelee
kufanyiwa kazi hadi kamati ya maendeleo ya jamii itakapokamilisha kazi yake na
kuwasilisha maoni yake bungeni.
Wakati huohuo bunge limepitisha
mswada wa sheria ya kuanzisha na kusimamia vituo vya pamoja mipakani wa mwaka
2015, ambapo akiwasilisha mswada huo, naibu waziri wa fedha Mhe.Adam Malima
amesema lengo la sheria hiyo ni kuondoa changamoto zilizopo sasa za kukaguliwa
mara mbili au zaidi kwa mizigo kwa ajili ya kukamilisha taratibu za forodha,
ucheleweshwaji wa mizigo na kuvuja kwa mapato.