Chama cha wamiliki wa daladala jijini Dar es Salaam-Darcoboa- kwa kimepanga kuhacha kuwatoza walimu wote wa shule za msingi na sekondari za serikali katika manispaa ya Kinondoni kuanzia machi 7 mwaka huu ikiwa ni kuungamkono uamuzi wa rais Dkt John Magufuli wa kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa Darcoboa Bwana Said Mabrouk amesema walimu wa shule za msingi na sekondari za serikali hawatotoza nauli kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa 2 asubuhi na wakati wa mchana ni kuanzia saa 9 hadi saa 11 jioni, na kusisitiza ambapo ametaka hamalshauri za manispaa kuweka utaratibu maalum wa vitambulisho vitakavyokuwa na picha za walimu hao.


Aidha akizungumza katika mkutano huo, mwenyekiti wa umoja wa wasafirishaji mkoa wa Dar es Salaam Bwana William Masanja amevitaka vyombo vya habari kutoa ushirikiano wa kutangaza mpango huo wa wamiliki wa daladala, umoja wa wasafirishaji, chama cha wafanyakazi madereva-Tadwu na serikali ili kuwawezesha walimu kufahamu wa shule za serikali kutambua fursa hiyo.

Chanzo: ITV

 
Top