Mtoto wa maajabu amezaliwa Wilaya ya karatu akiwa hana sehemu za haja kubwa na ndogo, ubongo ukiwa nje ya kichwa, hana kiganja cha mkono wa kushoto na mdomo umeungana na pua.
Mama wa mtoto, Grace Paul mkazi wa Kibaoni, Wilayani humo alisema mtoto huyo ni uzao wake wa tano kati ya watoto wake wanne alionao na alimzaa kwa upasuaji, April 22, mwaka huu katika Hospitali ya wilaya Karatu na kwamba hadi sasa bado yupo hai.
Alisema baada ya kujifungua mtoto huyo hakuamini kilichotokea badala yake
alitaka kutimua mbio na kumtelekeza hospitalini, hata hivyo daktari mfawidhi wa
hospitali hiyo alimshauri aondoke naye.Mama huyo anayeishi na mume, alieleza
kuwa hakuwa na shaka na ujauzito wake kama angeweza kuzaa kiumbe kama
hicho.
“Kwa kweli huyu kiumbe anaendelea vizuri nampa maziwa ila hawezi kunyonya
kama unavyouona mdomo wake umeungana na pua,” alisema kwa masikitiko makubwa
mama huyo.
Kwa upande wa mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Makyao alithibitisha
kuzaliwa kwa kiumbe huyo na alieleza kuwa mama wa mtoto alikuwa na upungufu wa
madini mwilini yaliyosababisha kupata ulemavu wa viungo.Hata hivyo alisema
kiumbe hicho hakitaishi kwa muda mrefu kama binadamu wengine na kitachukua muda
mfupi kuwa hai.
Chanzo Risasi Jumamosi