Waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amefanya ziara katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na kujionea msongamano mkubwa wa wagonjwa ambapo katika wodi ya wazazi ameshudia wagonjwa wakilala wawili katika kitanda kimoja na kumuagiza mganga mkuu wa hospitali hiyo Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lilo jirani na hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.
Chanzo: ITV